• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mpango Keisuke Honda kuibua vipaji Afrika Mashariki

    (GMT+08:00) 2017-11-28 12:43:59
    Nchi tatu za Afrika masharaki zitanufaika na zoezi la uibuaji pamoja na uendeleaji vipaji vya soka kwa vijana walio kwenye mazingira magumu na wakimbizi kwenye maeneo hayo, ambalo linaendeshwa na taasisi ya kimataifa ya Honda Estilo Corporation.

    Nchi hizo Rwanda ambako zoezi limeanza mwezi huu hadi mwezi Disemba, Kenya litakapoanza mwezi Januari hadi Aprili na Uganda ambako litaanza mwezi Aprili hadi mwezi mei, na mizunguko yote hii ikiwa ni awamu ya kwanza, hivyo likirudiwa tena mara kwa mara katika maeneo hayo ili kutimiza lengo la kupata wachezaji.

    Honda Estilo kampuni inayoongozwa na nyota wa mpira wa miguu kutoka Japan Keisuke Honda, akishirikiana na Will Smith ambaye ni mcheza filamu kutoka marekani, Yujiro Ohori ambaye ni bingwa wa gofu nchini Japan, Miyabi Onitsukai ambaye ni mshindi wa medali ya dhahabu katika michezo ya kwenye barafu, pamoja na Jaden Smith ambaye ni mwanamuziki na mwigizaji kutoka marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako