Waliofikwa na adhabu hiyo ni Aleksei Negodailo na Olga Vilukhina ambao ni washiriki katika michezo ya kuteleza kwenye barafu, na wengine Sergei Chiduniov, Dmitry Trunenkov na Yana Romanova ambao ni mahodari katika michezo ya kulenga shabaha.
Mpaka sasa IOC imewafungia wanamichezo 21 kutoka Urusi na imeendelea kuchukua maamuzi hayo kufuatia ripoti ya mamlaka ya kupambana na matumizi ya dawa za kuongeza nguvu michezoni WADA kuhusu Urusi.
Kamati hiyo pia inatarajiwa kutolea maamuzi ya eidha timu za urusi kushiriki au kutoshiriki katika Olimpiki ya majira ya baridi nchini Korea Kusini mwaka 2018.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |