• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waamuzi 18 Tanzania wakabidhiwa Beji za FIFA

    (GMT+08:00) 2017-11-28 12:45:38
    Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), limewatunuku utambuzi wa kimataifa Waamuzi wa Tanzania 18 ikiwa ni kuelekea msimu mpya wa mshindano mwaka 2018.

    Waamuzi walioteuliwa kwa upande wa wanaume ni Mfaume Ali, Elly Sasii, Emmanuel Mwandembwa na mkongwe Israel Nkongo na kwa upande wa wanawake wamo Jonesia Rukyaa na Florentina Zablon.

    Waamuzi Wasaidizi walipewa beji hizo (Wanaume) ni Soud Lillah, Mgaza Kunduli, Mohammed Mkono, Mbaraka Haule, Ferdinand Frank Chacha na Frank Komba na kwa wanawake ni Hellen Mduma, Dalila Jaffari, Jeneth Balama na Grace Wamala.

    Waamuzi wa mpira wa miguu unaochezwa ufukweni waliopata beji ni Jackson Steven Msilombo na Geofrey Tumaini Mwamboneko.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako