• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Everton waanza mazungumzo na Kocha Allardyce

    (GMT+08:00) 2017-11-28 12:46:22
    Klabu ya Everton imeanza mazungumzo na Sam Allardyce kwa ajili ya kuchukua mikoba ili kuinusuru timu hiyo ambayo imekuwa na msimu mbaya kuwahi kutokea katika historia yake na ikiwa katika hatari ya kupoteza nafasi ya kushiriki ligi kuu misimu ijayo.

    Everton imefungwa katika michezo mitano kati ya saba iliyocheza ikiwa chini ya meneja wake wa muda David Unsworth, ikiwaweka rekodi ya kufungwa magoli 9 katika michezo miwili.

    Sam Allardyce ambaye ni kocha wa zamani wa klabu za Bolton, Blackburn, Newcastle, Sunderland, West Ham and Palace manager, akiwa pia amewahi kuteuliwa kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Uingereza, ameendelea kutokuwa muwazi juu ya kuhamia klabuni hapo.

    Everton haijawa na kocha tangu imtimue Ronald Coeman Ocktoba 23 mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako