• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Emmanuel Okwi aachwa katika kikosi cha Uganda kitakachoshiriki mashindano ya Chalenji.

    (GMT+08:00) 2017-11-29 09:07:13

    Mshambuliaji wa Simba na kinara wa ufungaji katika Ligi Kuu Bara, Emmanuel Okwi ameachwa katika kikosi cha Uganda kitakachoshiriki mashindano ya Chalenji.

    Wakati Okwi mwenye mabao manane katika kikosi cha Simba akiachwa, Mganda mwenzake beki Juuko Murushid ndiye mchezaji pekee anayecheza nje ya Uganda aliyeitwa Cranes.

    Kocha wa zamani wa Simba, anayefundisha Cranes, Moses Basena ameita wachezaji 26 kambini watakaopungua na kubaki 23 kabla ya safari ya Nairobi Jumamosi hii wakati mashindano yatafunguliwa Jumapili Desemba 3.

    Mchezaji pekee anayecheza soka nje aliyeitwa ni beki wa Simba, Murushid ambaye alikuwepo katika kikosi cha Uganda Cranes kilichoshiriki fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2017) nchini Gabon.

    Okwi hajaifungia Simba tangu Oktoba 15, alipofunga bao la kusawazisha dhidi ya Mtibwa Sugar.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako