• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Jamii ya kimataifa yalaani jribio jipya la makombora lililofanywa na Korea Kaskazini

  (GMT+08:00) 2017-11-29 18:56:30

  Korea Kaskazini imethibitisha kuwa imefanya kwa mafanikio jaribio la kombora jipya aina ya ICBM mapema leo, ikiwa ni jaribio la karibuni zaidi la makombora ambalo limelaaniwa vikali na nchi na mashirika ya kimataifa.

  Jaribio hilo limefanyika wiki moja baada ya Marekani kuiweka tena Korea Kaskazini kwenye orodha ya nchi zinazofadhili ugaidi, na kuweka vikwazo vipya dhidi ya nchi hiyo.

  Rais Donald Trump wa Marekani ameongea kwa simu kwa nyakati tofauti na viongozi wa Japan na Korea Kusini juu ya jaribio hilo, ambapo waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe amerejea tena ahadi yake ya kukabiliana na tishio la makombora la Korea Kaskazini. Naye rais Moon Jae-in wa Korea Kusini akiilaani Korea Kaskazini kwa kuendeleza mpango wa kutenteneza makombora ya nyuklia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako