• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zimbabwe yajiondoa kwenye maichuano ya Cecafa ya Kenya

    (GMT+08:00) 2017-11-30 09:10:44

    Timu ya taifa ya Zimbabwe imejiondoa kwenye mashindano ya Cecafa yanayotarajiwa kuanza siku ya Jumapili nchini Kenya. Zimbabwe imetaja sababu kubwa ya kujiondoa kwake kuwa ni usalama.

    Zimbabwe na Libya zilialikwa kama wageni katika mashindano haya ambayo yanazijumuisha nchi za Afrika Mashariki na Kati ikiwemo bingwa mtetezi Uganda, wenyeji Kenya, Tanzania, Rwanda, Zanzibar, Burundi, Ethiopia na Sudan Kusini. Kocha wa Zimbabwe Sunday Chidzambwa, tayari alikwisha taja kikosi chake, lakini chama cha soka cha Zimbabwe kikasema kwa sasa hali ya Kenya hairuhusu. Hali ya usalama ya Kenya bado ni ya kusuasua kufuatia vurugu zilizotokea baada ya uchaguzi mkuu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako