• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China atoa pongezi kwa mkutano wa ngazi ya juu wa Asia na Pasifiki kuhusu masuala ya walemavu

    (GMT+08:00) 2017-11-30 18:18:34

    Mkutano wa ngazi ya juu wa tathmini ya katikati ya mambo ya walemavu katika kipindi kati ya mwaka 2013 hadi mwaka 2022 kati ya serikali za Asia na Pasifiki umefanyika hapa Beijing.

    Rais Xi Jinping wa China ametoa pongezi kwa mkutano huo akisema walemavu wana haki sawasawa na wengine kwenye jamii ya binadamu, na wakati dunia nzima inapohimiza maendeleo endelevu, inatakiwa kufuatilia zaidi walemavu.

    Rais Xi amesisitiza kuwa, China itaendelea kuendeleza mambo ya walemavu, kuwasaidia kujiendeleza na kujitajirisha kwa pamoja, na kusukuma mbele maendeleo ya pamoja ya masuala ya walemavu duniani ikiwemo Asia na Pasifiki.

    Amesema anatarajia mkutano huo utatoa mchango mpya kwa kuongeza manufaa kwa walemavu katika kanda hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako