• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Jumuiya ya kimataifa yaafikiana kuhusu kuondolewa kwa dharura kwa wahamiaji haramu nchini Libya

  (GMT+08:00) 2017-11-30 19:43:02

  Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa jana usiku huko Abijan, Cote d'Ivoire amesema, nchi tisa za Ulaya na Afrika, Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika zimeafikiana kuondolewa kwa dharura kwa wahamiaji haramu walioko nchini Libya.

  Rais Macron amesema hayo katika mkutano wa 5 wa kilele wa Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika uliofunguliwa jana huko Abidjan. Wajumbe kutoka Ujerumani, Italia, Hispania, Ufaransa, Chad, Niger, Libya, Jamhuri ya Kongo, Morocco na Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika wamekubali kufanya operesheni ya dharura ya kuwasaidia wahamiaji wa Afrika kuondoka Libya.

  Rais Macron amesema, operesheni hiyo itafanyika ndani ya siku kadhaa au wiki kadhaa, kwa kuwa wasafirishaji haramu wa binadamu wanahusiana na kundi la ugaidi, wanapaswa kukamatwa na kuadhibiwa kwa mujibu wa sheria.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako