• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yachangia shughuli za kinga na udhibiti wa maambukizi ya ukimwi barani Afrika

    (GMT+08:00) 2017-12-01 15:29:46

      

    Tarehe 1 Desemba mwaka huu ni Siku ya 30 ya Ukimwi Duniani. Afrika ni eneo linaloathiriwa zaidi na maambukizi ya ukimwi duniani, takwimu zilizotolewa tarehe 20 Novemba na Shirika la kupambana na Ukimwi la Umoja wa Mataifa zinaonesha kuwa, hivi sasa watu milioni 37 wanaishi na virusi vya ukimwi duani, na milioni 26 kati yao wanatoka Afrika. Hapa nchini China, idadi ya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi, vilevile imekuwa ikiendelea kuongezeka katika miaka ya karibuni.

    Tangu Mkutano mkuu wa 18 wa Chama cha Kikomunisti cha China uliofanyika miaka mitano iliyopita, chama hicho kinachoongozwa na rais Xi Jinping kinatilia maanani sana kinga na udhibiti wa maambukizi ya ukimwi. Mwaka 2012 mnamo Siku ya Ukimwi Duniani, baada ya rais Xi Jinping kuingia madarakani, alienda hospitali moja mjini Beijing, kuwatembelea wagonjwa wa ukimwi, na kuzungumza nao uso kwa uso, na hata kushikana nao mikono. Rais Xi alieleza kwamba, ugonjwa wa ukimwi sio wa kutisha, kinachotosha ni ubaguzi dhidi ya watu wenye virusi vya ukimwi, ambao wote ni dada na kaka zetu, na jamii yetu inatakiwa kuwatunza kwa upendo.

    Wakati huo huo China pia inazisaidia nchi za Afrika kwa juhudi kubwa katika mapambano dhidi ya ukimwi. Serikali hadi mashirika ya kiraia na kampuni, zote zinatoa mchango kwa ajili ya ushirikiano wa shughuli hii kati ya China na Afrika. Bw. Feng Yong, naibu mkurugenzi wa idara ya ushirikiano wa kimataifa katika Kamati ya afya na uzazi wa mpango ya China anajulisha kuwa, China inaunga mkono nchi za Afrika katika ujenzi wa utaratibu wa kinga na udhibiti wa maambukizi ya ukimwi, na kutoa mchango kwa ajili ya maendeleo ya shughuli za afya barani Afrika.

    "Hivi sasa, vikundi vya matibabu kutoka China vipo katika nchi 43 barani Afrika, na madaktari wapatao elfu moja wanafanya kazi barani humo, na watu wengi waishio na virusi vya ukimwi wametibiwa na kufanyiwa upasuaji nao. Vilevile China imetoa mafunzo na misaada ya masomo kwa wataalamu wa Afrika wenye ujuzi kuhusu kinga na udhibiti wa maambukizi ya ukimwi, na mwaka huu wataalamu 45 kutoka Afrika wamefundishwa hapa China. Mbali na hayo, tumeandaa shughuli nyingine za matangazo, mnamo mwaka 2016 tuliwaalika yatima ambao wazazi wao walifariki kwa ugonjwa wa ukimwi kuja China kushiriki kwenye shughuli za kambi za majira ya joto."

    Mashirika ya kiraia na kampuni za China vilevile zimekuwa na ushirikiano na mashirika ya Umoja wa Mataifa, zikitumia vya kutosha nguvu yao na kuchangia shughuli za kinga na udhibiti wa maambukizi ya ukimwi barani Afrika. Mwaka 2015 watu sita kutoka Baraza la biashara kati ya China na Afrika na Mfuko wa maendeleo kati ya China na Afrika, na wanafunzi watatu nchini China walianzisha mradi unaoitwa Mfuko wa "Kuongeza upendo na kupungua UKIMWI", ambao unalenga kuwasaidia waja wazito wenye virusi vya ukimwi kuhudumiwa kwenye wadi ya wazazi, ili kuzuia kuwaambukiza virusi watoto wachanga. Wang Ruoqing, msichana anayejitolea wa jumuiya ya kupambana na UKIMWI ya CHina, ambaye pia ni mwanafunzi wa shule ya sekondari mjini Beijing ni mmoja wa aliyeanzisha mradi huo, anasema:

    "Kuwafanyia wengine mambo madogo pia ni jambo zuri. Miaka miwili imepita tangu mfuko wa 'Kuongeza Upendo na Kupunguza UKIMWI' uanzishwe mwaka 2015. Katika miaka hiyo miwili, mfuko huo uliozinduliwa na watu tisa umeshirikisha watu zaidi ya milioni 2 na kutoa dola zaidi ya milioni 2 za kimarekani. Hivi sasa tunaendelea kufanya juhudi, ili kupanua mfuko huo na kuinua ushawishi wake."

    Mwezi Machi mwaka jana, Baraza la biashara kati ya China na Afrika lilisaini makubaliano na jumuiya ya wake wa marais wa nchi za Afrika kwenye mapambano dhidi ya UKIMWI, OAFLA, mpaka sasa limetoa ufadhili wa thamani ya dola za kimarekani laki tatu kwa mara tatu jumla, ambao utatumika katika kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi toka kwa mama kwenda kwa mtoto, na kupunguza idadi ya wanawake wanapojifungua wenye virusi vya UKIWMI nchini Kenya, Tanzania, Uganda na kwenye nyingine za Afrika. Bw. Feng Qiang, anayeshughulikia mradi huo kutoka Baraza la biashara kati ya China na Afrika anatufahamisha:

    "Hivi sasa utekelezaji wa kipindi cha kwanza cha mradi huo umekamilika, ambao unaunga mkono miradi husika ya matangazo ya kinga na udhibiti wa UKIMWI, huduma kwa watoto wenye hali duni ya maisha, upimaji wa virusi vya UKIMI na kukomesha maambukizi ya virusi hivyo kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto. Kwa mujibu wa ripoti zilizotolewa, watu 10402 wamenufaika na mradi wetu katika sekta za upimaji, virutubisho, matibabu na elimu."

    Ikiwa ni kampuni inayofanya biashara ya matangazo ya televisheni ya kidigitali katika nchi zaidi ya 30 barani Afrika, StarTimes pia inashirikiana na Shirika la kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa kutangaza ujuzi wa kinga ya ukimwi kupitia channel zake barani Afrika. Kwa mujibu wa makubaliano yaliyosainiwa na tawi la kampuni hiyo nchini Uganda na shirika hilo mwezi mei mwaka huu, pande hizo mbili zitatekeleza ushirikiano wa kuwaelimisha vijana wa Uganda ujuzi wa kinga na udhibiti wa maambukizi ya ukimwi. Meneja wa tawi la Uganda la StarTimes Bw. Wang Xiaoqing anaeleza:

    "Ya kwanza ni kutangaza video fupi zinazotolewa na UNAIDS kupitia vituo vyetu vya televisheni. Lingine tumeweka picha za kutangaza mapambano dhidi ya UKIMWI kwenye jukwaa letu la mwongozo wa vipindi vya televisheni. Kwa upande mwingine, kila ukumbi wetu wa huduma una eneo maalumu unaotangaza ujuzi kuhusu UKIMWI. Aidha, tumefadhili klabu mbili za soka huko, huku tuikishirikiana na UNAIDS pamoja na klabu hizo kuandaa shughuli za kutangaza mapambano dhidi ya UKIMWI. Hii pia ni njia ya moja kwa moja ya kutangaza ujuzi kwa vijana. Mbali na hayo, tumeandaa shughuli mbalimbali za muziki, kwa mfano hivi karibuni tutafanya maonesho ya muziki yatakayotangaza ujuzi kuhusu kupambana na UKIMWI. Tutaendelea kufanya shughuli zinazohusu kupambana na UKIMWI, ili kutekeleza jukumu la kijamii la kampuni. "

    Mwezi Juni mwaka jana, nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zilipitisha "Tangazo la siasa kuhusu virusi vya ukimwi na suala la ukimwi", ambalo nchi mbalimbali zimeahidi kukomesha maambukizi pa kubwa ya ugonjwa huo ifikapo mwaka 2030. Mwezi Agosti mwaka huu, StarTimes na Shirika la kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa walikutana mjini Beijing, ambapo walijadili kuondoa athari ya maambukizi ya ukimwi na kutimiza lengo la "kukomesha maambukizi pa kubwa ya ukimwi" barani Afrika. Mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo Bw. Michel Sidibe alipohojiwa na vyombo vya habari nchini Uganda, alisema anafurahia ushirikiano kati ya shirika lake na kampuni ya China katika mapambano dhidi ya ukimwi.

    "Tumefurahishwa sana na ushirikiano huu na StarTimes, tunaitazama StarTimes kama njia ya mawasiliano na kuwafikia watu ambao wamebaki nyuma, ni sehemu pia ya falsafa ya kufikia malengo ya maendeleo endelevu. Startimes pia ni njia ya kisasa ya kuwapelekea watu ufahamu, uhusiano huu ni ufunguo kwetu, ni muhimu kwa kuwa utatusaidia kuhamasisha watu juu ya kinga, watachukua hatua stahiki za kujikinga. "

    Katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na matangazo yaliyotolewa na kampuni za China, watu wa Afrika wana ufahamu zaidi juu ya virusi vya ukimwi, na pia ubaguzi dhidi ya watu wanaoishi na virusi hivyo umepungua. Kenya ni moja ya nchi sita zinazoathiriwa zaidi na maambukizi ya ukimwi barani Afrika, mwaka 2016 watu wapatao milioni 16 nchini humo waliambukuziwa virusi vya ukimwi, idadi inayochukua asilimia 6 ya watu wa nchi hiyo, huku zaidi ya theluthi mbili wa walioambukizwa wanatumia dawa za ARVs. Naibu mkurugenzi wa Kamati ya udhibiti wa ukimwi ya taifa la Kenya Bw. Regina Ombama alimwambia mwandishi wetu wa habari kuwa, serikali na kampuni za China wametoa misaada mikubwa kwa ajili ya kinga na udhibiti wa ukimwi nchini Kenya, anatumai kuwa China itaendelea kuzisaidia nchi za Afrika ikiwemo Kenya kukamilisha utaratibu wa huduma za kinga na tiba ya ukimwi, ili kuwanufaisha jamaa wengi zaidi.

    "Sasa tunaona serikali ya China ikiingia kwenye maswala ya afya hasa wakisaidia na vifaa vya matibabu. Eneo moja ambako nimefurahia kuhusu msaada wa China ni katika 'Kampeni ya Beyond Zero' ambayo ilianzishwa na mke wa rais Bi Magaret Kenyatta, ambapo serikali ya China ilisaidia katika kutunza afya za mama na watoto wanaozaliwa na ambayo ni sehemu muhimu katika harakati zetu za kukabiliana na HIV. Pia tunatarajia kushirikiana na China kwenye sekta ya elimu hasa sayansi na teknolojia, ili kufanya kazi nao kutambua njia za kuangamiza kabisa janga la ukimwi hata kabla ya mwaka 2030."

    Katika siku za mbele, mbali na kutoa ufadhili na matangazo husika, kampuni za China vilevile zinaweza kufanya kazi kubwa katika kutoa dawa za kudhibiti ukimwi. Mkuu wa mradi wa utunzaji jamii wa Baraza la biashara kati ya China na Afrika Bw. Feng Qiang anajulisha kuwa, kampuni moja ya utengenezaji dawa nchini China tayari imeahidi kulifadhili baraza lake dawa za kudhibiti ukimwi zenye thamani ya dola za kimarekani laki tatu kila mwaka, dawa hizo zikifanikiwa kuingia kwenye soko la Afrika kwa kufuata sheria husika, Baraza la biashara kati ya China na Afrika litazitoa bure kwa watu wa Afrika. Katika miaka ya hivi karibuni, serikali ya Tanzania imekuwa inatilia maanani siku hadi siku ushirikiano wa kimataifa katika kinga na udhibiti wa maambukizi ya ukimwi. Balozi wa Tanzania nchini China Bw. Mbelwa Kairuki anatuelezea matumaini yake kwamba, China itaimarisha ushirikiano kati yake na Tanzania katika sekta ya afya ya umma, haswa kazi ya kinga na udhibiti wa maambukizi ya ukimwi.

    "Ushirikiano wa Tanzania na China kwenye sekta ya afya upo katika Nyanja mbalimbali, nyanja ya kinga, Nyanja ya tiba. Huu ugonjwa wa ukimwi ni ugonjwa ambao umetuathiri sana barani Afrika na Tanzania ikiwemo. China sasa hivi ina namna mbili za kusaidia, kwanza wanachangia kwenye ule mfuko wa kimataifa wa ukimwi ambao Tanzania ni moja ya nchi ambazo zinanufaika na mfuko ule. Lakini la pili, China inaendelea kutusaidia kwa kutengeza dawa za bei nafuu ambazo zinapatikana kwenye nchi zetu, kwa sasa wanatengeza zao jipya la tatu la dawa za kufubaza makali ya virusi vya ukimwi (ARVs'), ambazo zimekuwa zikisaidia watu wengi kuishi maisha bora baada ya kuathirika, lakini tunachotaka kwenda mbele huko, tufikie hatua China watusaidie kuwekeza kwenye viwanda vya dawa, zile dawa zitengenezwe pale pale Tanzania na Afrika."

    Hivi sasa shughuli za kinga na udhibiti wa maambukizi wa ukimwi duniani zinakabiliana na changamoto kubwa, serikali ya China inazingatia sana shughuli hizo na kushiriki kwa juhudi kubwa kwenye ushirikiano wa kimataifa, ili kujitahidi kutimiza lengo la kukomesha maambukizi makubwa ya ukimwi pamoja na nchi nyingine, kabla ya mwaka 2030, na kazi muhimu zaidi iko barani Afrika. Mjumbe wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Ukimwi nchini China Bibi Amakobe Sande anasema, shirika lake linatumai na kuunga mkono kampuni za China kutengeneza dawa za kudhibiti maambukizi ya ukimwibarani Afrika, ili watu wanaoishi na virusi vya ukimwi waweze kupata dawa kwa bei nafuu zaidi kwa urahisi.

    "Afrika huzalisha asilimia tatu tu ya dawa zinazozihitajika katika bara zima, asilimia tatu tu. Hivyo tunasema, tukiwa kama sehemu ya FOCAC jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika, na tukiwa sehemu ya Belt and Road jukwaa la kimataifa la Maendeleo ya Ujenzi Miundo Mbinu, kwa nini sasa tusishirikiane na serikali ya China kusaidia uzalishaji wa dawa ndani ya bara la Afrika. Na sihitaji kueleza jinsi jambo hili litakavyokuwa na manufaa kwa pande zote. Hivyo, kwa muda sasa Shirika la kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa limeendelea na mjadala kuhusu suala zima ushirikiano katika masuala ya afya baina ya China na Afrika. Tunataka kuhakikisha ARVs zinazotengezwa China, ziruhusiwe kuuzwa Afrika na nchi nyingine zenye kipato cha chini."

    Mke wa rais Xi Jinping wa China Bibi Peng Liyuan anajulikana duniani akiwa "balozi wa kinga na udhibiti wa ugonjwa wa Kifua Kikuu na ukimwi" wa Shirika la afya WHO. Mwezi Desemba mwaka juzi, Bibi Peng Liyuan pamoja na wake wa viongozi wa nchi 10 za Afrika, walitoa pendekezo la pamoja linaloitwa "China na Afrika zashikamana kwa ajili ya mustabakabli wa kuondoa virusi vya ukimwi". Na mwezi Januari mwaka huu, alipohutubia hafla ya kurefusha muda wake wa balozi, Bibi Peng Li Yuan anasema:

    "Nilipoteuliwa kuwa balozi wa WHO miaka mitano na nusu iliyopita, nilisema nitatoa mchango wangu katika kazi kubwa za WHO za kuokoa maisha kutokana na vifo vinavyosababishwa na virusi vya Ukimwi, pamoja na kuwasaidia wale walioko kwenye mazingira hatarishi. Kabla ya hapo nilikuwa balozi wa China katika masuala ya Ukimwi kwa muda wa miaka mitano, hivyo nilikuwa nafahamu ni kitu gani tunachotakiwa kufanya, na kwamba nini kingetokea endapo tusingefanya kazi kwa bidii na kwa wakati mwafaka. Hii si vita kwa ajili ya kuwakomboa ya wale walioathirika tu, bali ni vita dhidi ya ustawi wa maisha ya binadamu katika siku za usoni, ni lazima tufanikiwe, na hakika tutashinda. "

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako