• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaeneza elimu ya kimapenzi katika shule na vyuo vikuu

    (GMT+08:00) 2017-12-01 17:24:00

    Leo tarehe mosi, Disemba ni siku ya 30 ya Ukimwi duniani. Hadi kufikia Juni mwaka 2017, idadi ya watu waliothibitishwa kuambukizwa virusi vya Ukimwi au wagonjwa nchini China imefikia laki 7.18, na njia kuu ya maambukizi ni kujamiiana, huku njia ya kuwekewa damu ikikomeshwa kabisa. Maambukizi kwa vijana na wazee yanaongezeka kwa kasi. Wataalamu wametoa wito wa kuimarisha elimu ya jinsi katika shule na vyuo vikuu, ili kupunguza maambukizi ya ukimwi kwa wanafunzi.

    Takwimu zilizotolewa na kamati ya afya na uzazi kwa mpango ya China zinaonesha kuwa, maambukizi ya virusi vya Ukimwi yaliyoripotiwa kuanzia Januari hadi Julai mwaka huu ni elfu 68, na kuongezeka kwa asilimia 8.5 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu. Takwimu hizo pia zinaonesha kuwa kiwango cha maambukizi ya virusi vya Ukimwi nchini China ni asilimia 0.05, na kati ya mikoa yote 31 nchini China, kiwango hicho katika mikoa mitano ya Yunan, Guangxi, Sichuan, Xinjiang na Chongqing kimezidi asilimia 0.1.

    Katika miaka ya hivi karibuni, ongezeko la maambukizi kati ya wanafunzi vijana linafuatiliwa na pande mbalimbali. Takwimu zinaonesha kuwa maambukizi kati ya wanafunzi vijana yanachukua kati ya asilimia 14 na 15 ya maambukizi yote nchini China. Mkurugenzi wa ofisi ya kueneza elimu ya kupambana na Ukimwi kwa vijana na watoto ya China Zhang Yinjun amesema, kuwafundisha vijana na watoto kuhusu elimu ya jinsia ni muhimu sana. Anasema,

    "Vijana na watoto wanahitaji wapenzi wanapokua, wakati huo huo wanakuwa hawajapata elimu ya kutosha kuhusu afya ya jinsia. Katika miaka ya hivi karibuni, maambukizi ya virusi vya Ukimwi yanaongezeka katika shule na vyuo vikuu, ambapo zaidi ya asilimia 95 ya maambukizi hayo yanatokana na njia ya kujamiiana."

    Ili kukabiliana na changamoto hiyo, China imefanya juhudi katika sehemu mbalimbali. Kuanzia mwaka 2015, vyuo vikuu 94 nchini China vimeanza majaribio ya kueneza elimu ya kinga Ukimwi na elimu ya mambo ya jinsia. Aidha, kutokana na mradi wa kueneza elimu ya kinga ya Ukimwi kwa vijana na watoto, China imejenga kituo cha kueneza elimu husika katika vyuo vikuu, shule na shule za chekechea zaidi ya 900.

    Xu Xiwen ni mwanafunzi wa darasa la tano wa shule ya msingi ya Wannianhuacheng mjini Beijing. Amepata elimu nyingi kupitia kituo hicho. Anasema,

    "Virusi vya Ukimwi vinaambukizwa kati ya watu. Kwa mfano kama mja mzito ana virusi, mtoto wake anaweza kuambukizwa wakati anapozaliwa. Kama mtu akitumia sirinji ya kupiga sindano pamoja na mwingine mwenye virusi vya Ukimwi, yeye atakuwa na virusi."

    Mkuu wa shule hiyo Bw. Liu Xianyang anaona kuimarisha elimu ya msingi kuhusu afya ya jinsia shuleni kutawasaidia watoto wawe na mwamko wa kujikinga dhidi ya Ukimwi. Anasema,

    "Tunaeneza elimu ya kinga dhidi ya virusi vya Ukimwi, pamoja na elimu ya jinsia. Zamani watu wengi wanaona maradhi hayo yako mbali na watoto wa shule ya msingi, lakini ni afadhali tuwafahamishe watoto mapema kuhusu kinga ya Ukimwi katika akili za watoto."

    Mwakilishi wa Shirika la Mipango ya Ukimwi la Umoja wa Mataifa nchini China Bi Amakobe Sande amesema, China imepigia hatua kubwa katika kukinga Ukimwi kati ya vijana. Anasema,

    "Hadi kufikia mwishoni mwa 2016, kulikuwa na maambukizi mapya zaidi ya milioni 1.8 ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi duniani, na lengo letu ni kupunguza kuwa chini ya laki 5 hadi kufikia mwaka 2020. Ingawa hatujakuwa na chanjo ya Ukimwi hadi sasa, lakini tuna hatua mbalimbali za kukinga maradhi hayo. Tunatumai kuwa tutaangamiza Ukimwi hadi kufikia mwaka 2030."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako