• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa wito kwa vyama vya siasa duniani kushirikiana kujenga dunia bora

    (GMT+08:00) 2017-12-02 16:11:47

    Rais Xi Jinping wa China ambaye pia ni katibu mkuu wa kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC amesema vyama vya siasa vya nchi mbalimbali vinatakiwa kuzidisha hali ya kuaminiana, kuongeza mawasiliano na uratibu kati yao na kutafuta kujenga uhusiano wa aina mpya wa vyama.

    Rais Xi ameyasema hayo alipotoa hotuba yenye ujumbe usemao "kushikana mikono kujenga dunia bora zaidi" katika mkutano wa ngazi ya juu wa mazungumzo kati ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC na vyama vya siasa duniani uliofanyika jana hapa Beijing.

    Pia amesema vyama vya siasa duniani vinatakiwa kushikilia kanuni za kutafuta mambo sawa na kuweka kando tofauti kati yao, kuelewana na kufundishana, na pia kujenga mitandao ya aina na ngazi mbalimbali ya mawasiliano na ushirikiano kati yao ili kuchangia nguvu zaidi katika kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja. Akizungumzia Chama cha Kikomunisti cha China CPC, rais Xi amesema

    "CPC ni chama kinachowatafutia neema watu wa China na kulistawisha taifa la China, pia ni chama kinachofanya juhudi kwa ajili ya maendeleo ya binadamu. Tunapaswa kufanya vizuri mambo yetu, hatua ambayo ndio mchango kwa ajili ya kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja. Tunatakiwa kusukuma mbele maendeleo ya China ili kutengeneza fursa nyingi zaidi kwa dunia. Sisi "hatuingizi" ndani muundo wa nchi za nje, wala "hatusafirishi" nje muundo wa China, na hatuzitaki nchi nyingine "kunakili" vitendo vya China. CPC itaendelea kutoa mchango kwa ajili ya amani, utulivu, maendeleo na mabadilishano ya ustaarabu wa aina mbalimbali duniani."

    Rais Xi pia amesema katika miaka mitano ijayo, CPC itatoa fursa kwa watu elfu 15 kutoka vyama vya siasa vya nchi nyingine duniani kuja China, na pia amependekeza kufanya mkutano wa ngazi ya juu wa mazungumzo kati ya CPC na vyama vya siasa duniani kufanyika kila baada ya muda fulani, ili kuufanya kuwa jukwaa la ngazi ya juu la mazungumzo ya kisiasa lenye uwakilishi na ushawishi mkubwa wa kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako