• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanafunzi 20 wa Kenya wapata ufadhili wa masomo kutoka ubalozi wa China

    (GMT+08:00) 2017-12-02 17:47:32

    Ubalozi wa China nchini Kenya jana katika Chuo Kikuu cha Nairobi umetoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi 20, na kila mmoja wao amepata dola za kimarekani elfu moja.

    Akitoa hotuba kwenye hafla ya kutoa ufadhili, balozi Liu Xianfa ametoa wito kwa vijana wa Kenya kufanya juhudi zenye malengo na kuchangia nguvu kwa ajili ya utimizaji wa dira ya Kenya ya mwaka 2030. Amesema ubalozi wa China nchini humo utaendelea kuunga mkono taasisi za elimu, kuwasaidia vijana kutimiza ndoto zao.

    Naye mkuu wa chuo kikuu cha Nairobi Peter Mbithi ametoa shukrani kwa ubalozi wa China na kuahidi kuwa chuo kikuu hicho kitatekeleza ipasavyo mipango ya miradi mbalimbali inayoungwa mkono na serikali ya China.

    "Ufadhili wa Masomo wa Balozi wa China" ulizinduliwa mwaka 2013 na ubalozi wa China nchini Kenya, na unalenga kuwasaidia wanafunzi bora wanaotoka familia yenye hali ngumu ya kiuchumi, na mpaka sasa wanafunzi 98 wamepata ufadhili huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako