• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan Kusini kujiunga na Mkataba wa Silaha za Kemikali

    (GMT+08:00) 2017-12-02 17:47:58

    Sudan Kusini itakuwa nchi mwanachama wa Mkataba wa Silaha za Kemikali, CCW na kujiunga na Shirika la Kuzuia Silaha za Kemikali Duniani, OPCW.

    Hayo yametangazwa na mkurugenzi mkuu wa ushirikiano wa kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ya Sudan Kusini Moses Akol Ajawin kwenye kikao cha 22 cha Mkutano wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Silaha za Kemikali.

    Naye mkurugenzi mkuu wa OPCW amepongeza uamuzi huo wa Sudan Kusini na kutaka nchi za Misri, Israel na Korea Kaskazini ambazo hazijajiunga na Shirika hilo kuungana na nchi nyingine duniani katika kutokomeza silaha zote za kemikali.

    Habari nyingine zinasema waasi 92 wameuawa na jeshi la Sudan Kusini katika mapambano mapya yaliyotokea katika mji wa kaskazini wa Leer, kusini mwa jimbo la Liech.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako