• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Mnangagwa wa Zimbabwe afanya mabadiliko ya baraza la mawaziri

    (GMT+08:00) 2017-12-03 16:22:28

    Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe siku ya jumamosi amelifanyia mabadiliko madogo baraza la mawaziri ili kuhakikisha yanafuata katiba, jinsia na mahitaji mengine.

    Katika uteuzi wake, Mnangagwa amemuacha waziri wa elimu ya msingi na sekondari Lazarus Dokora siku moja baada ya kumteua na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa naibu wake Paul Mavhima, katika uteuzi huo pia kuna maafisa wawili wa jeshi.

    Kulingana na katiba ya nchi hiyo, Mnangagwa ana nafasi za uteuzi wa watu watano ambao si wabunge kwenye baraza la mawaziri lakini amefanya uteuzi wa viongozi saba, ambao wawili kati yao amewaondoa jumamosi.

    Alhamisi ya wiki iliyopita, Rais Mnangagwa aliteua mawaziri 22 kwenye baraza la mawaziri, hatua ambayo ilivutia maoni tofauti toka kwa umma huku mawaziri wapya wataapishwa Disemba 4 mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako