• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa Somalia, AU na AMISOM kufanya mkutano wa usalama

    (GMT+08:00) 2017-12-04 08:54:43

    Somalia leo itafanya mkutano wa usalama ili kutafuta uungaji mkono wa mahitaji ya maofisa wa usalama kufuatia kuondoka kwa askari wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika AMISOM.

    Mkutano huo ambao unaitishwa na Tume ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa nchini Somalia AMISOM ikishirikiana na Serikali ya Somalia, pia utajadili njia za kuifadhili sekta ya usalama nchini humo na hatua ijayo ya muda wa mpito wa AMISOM.

    Kwenye taarifa iliyotolewa Mogadishu, mjumbe maalum wa mwenyekiti wa Kamati ya AU nchini Somalia Bw Francisco Madeira amesema mkutano huo utaangalia kwa kina hatua iliyopigwa hadi sasa katika nyanja za siasa na usalama. Amesema mafanikio yatapimwa kwa kuangalia maamuzi gani muhimu yatatolewa kuwezesha AMISOM kuleta ufanisi na kuimarisha operesheni za mapambano dhidi ya kundi la al-Shabaab.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako