• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawaziri wa nchi za Afrika wazindua mpango wa kushirikisha wanawake katika sekta ya nishati

    (GMT+08:00) 2017-12-04 09:30:42

    Mawaziri wa nchi za Afrika wamezindua mpango mpya unaolenga kuwashirikisha wanawake katika sekta ya nishati.

    Shirika la mfumo wa wajasiriamali wanawake wa nishati barani Afrika AWEEF lililozinduliwa jana kwenye Mkutano wa mawaziri kuhusu mazingira AMCEN uliofanyika mjini Nairobi, linalenga kuhimiza serikali za nchi za Afrika na wadau wa maendeleo kutoa ahadi za kisiasa ili kuvutia uwekezaji katika kuongeza upatikanaji wa nishati safi na ya bei nafuu barani humo.

    Waziri wa maliasili na mazingira wa Kenya Bibi Judi Wakhungu, amesema kuwawezesha wajasirimali wanawake waoneshe uwezo wao katika sekta ya nishati endelevu ni muhimu katika kutimiza malengo ya maendeleo endelevu pamoja na ajenda ya kuelekea mwaka 2063 ya Umoja wa Afrika, pia amesema kuwa AMCEN itatoa msaada muhimu kwa mpango huo na kuhimiza washirika wengine kujiunga nayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako