• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Gofu: Tiger Woods ashinda nafasi ya Tisa Bahamas

    (GMT+08:00) 2017-12-04 10:14:23

    Licha ya kukosa ubingwa katika mashindano ya Bahamas yaliyomalizika jana, wachambuzi wa masuala ya mchezo wa Gofu, wamesema huenda Tiger Woods akarejea katika kiwango cha kuridhisha kutokana makali aliyoyaonyesha tangu aanze mazoezi na hatimaye ushiriki wake katika mashindano.

    Woods ambaye amecheza kwa mara ya kwanza tangu atangaze kujiondoa mwezi februari mwaka huu, alishika nafasi ya tisa kati ya wachezaji 19 walioshiriki michuano hiyo, na bingwa alikuwa Rickie Fowler wa Marekani.

    Na nafasi ya pili ikienda kwa Charley Hoffman (Marekani), ya tatu kwa Tommy Fleetwood (Uingereza), Jordan Spieth (Marekani) akishika nafasi ya nne, na nafasi ya tano ikienda kwa Hideki Matsuyama (Japan).

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako