• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasema maazimio ya Baraza la Usalama ni wajibu wa kimataifa unaotakiwa kutekelezwa na pande mbalimbali

    (GMT+08:00) 2017-12-04 16:50:00

    China inapinga kithabiti Korea Kaskazini kuendeleza majaribio ya makombora ya nyuklia kwa kupuuza maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kusema China inatekeleza maazimio hayo kikamilifu kwa makini,

    Hayo yamesemwa na waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi leo hapa Beijing alipojibu swali kuhusu hali ya Peninsula ya Korea katika mkutano na waandishi wa habari. Bw. Wang amesema China inapinga vitendo vyote vinavyozidisha hali ya wasiwasi katika peninsula ya Korea, na inashikilia kusukuma mbele mazungumzo ya amani kwa mujibu wa matakwa ya mikutano ya Baraza la Usalama.

    Bw. Wang ameongeza kuwa, China ina msimamo wazi kuhusu mapendekezo na maoni mapya yaliyotolewa na pande mbalimbali, lakini pande hizo zina wajibu wa pamoja wa kufuata kanuni na malengo ya maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kwani maazimio hayo ni uamuzi wa pamoja wa jamii ya kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako