• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa mpango wa kupunguza umaskini kwenye mkutano wa Internet duniani

    (GMT+08:00) 2017-12-04 18:45:53

    Kongamano kuhusu kupunguza umaskini kupitia Internet la mkutano wa 4 wa Internet duniani limefanyika leo asubuhi mjini Wuzhen, China, na kuhudhuriwa na wajumbe wa mashirika ya kimataifa, serikali za Marekani, Ghana, Nepal na Ethiopia, wanaviwanda, na watu walioondokana na umaskini nchini China.

    Kwenye kongamano hilo, wajumbe wamebadilisha maoni kuhusu utekelezaji wa Ajenda ya Maendeleo Endelevu ya 2030 ya Umoja wa Mataifa, njia ya kuwasaidia watu maskini kupitia Internet, kupunguza pengo la kidijitali, na kuwasaidia watu maskini kwa mujibu wa hali yao ya kipekee. Wajumbe hao pia wamesifu mafanikio ya China katika kuwasaidia watu kuondokana na umaskini kupitia Internet, na kusema China imetoa uzoefu na mpango wa kazi ya kupunguza umaskini duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako