• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya:Bei za umeme kupungua kuanzia sasa

  (GMT+08:00) 2017-12-04 18:56:27

  Wakenya watapata nafuu ya matumizi ya umeme kuanzia wiki hii.

  Hii ni kwa mujibu wa tume ya kawi nchini Kenya ERC iliyotangaza bei ama tarifu mpya za ruzuku kutoka kwa serikali.

  Watakaonufaika pakubwa ni mashirika ya viwanda yanayotumia umeme wa viwango vikubwa ambao kwa sasa ,watalipa bei ya chini kuanzia saa nne usiku hadi saa kumi na mbili asubuhi kila siku.

  Kampuni ya Kenya Power itapunguza bei ya shihilingi 5 kwa kila kilowati moja kwa saa ,kutoka shilingi saba za hapo awali.

  Waendeshaji viwanda watalipa shilingi 7 kwa kila uniti kutoka shilingi 9.20.

  Pavel Oimeke kaimu, mkurugenzi mkuu wa tume ya kawi nchini Kenya amesema bei hizo mpya zitaimarisha ukuwaji wa viwanda na pia kuwasaidia wakenya kupunguza gharama za maisha.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako