• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya:Utalii wanoga msimu wa likizo

  (GMT+08:00) 2017-12-04 18:58:06

  Hoteli za kitalii katika mkoa wa pwani nchini Kenya zimerekodi ongezeko kubwa la idadi ya watalii mwezi Novemba na Disemba.

  Kulingana na mwenyekiti wa shirikisho la utalii nchini Kenya Mohamed Hersi,watalii wameongezeka kufuatia likizo za disemba,mikutano na watalii wa kutoka nje wanaouzuru kutalii mbuga za wanyama na hali ya kiangazi.

  Hersi amesema wamefurahishwa na ongezeko hilo baada watalii kupungua kwa kiasi kikubwa wakati wa uchaguzi mkuu wa urais.

  Mombasa pekee,watalii wameongezeka kwa asilimia 10 kutoka 60 kwa mwezi mmoja tu.

  Mwaka huu asilimia 80 hadi 100 ya watalii wanatajiwa kuwasili Mombasa kwa msimu wa krismasi na mwaka mpya.

  Aidha asilimia 40 ya watalii wa msimu huu wanawasili kutoka India,China,Marekani na Uingereza.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako