• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rwanda;Maharagwe yanaboresha akili ya binadamu,utafiti

  (GMT+08:00) 2017-12-04 18:59:02

  Ulaji wa maharagwe ya madini mengi ya protini huimarisha uwezo wa kuweka kumbukumbu kwa wanawake kulingana na utafiti mpya uliofanywa Marekani katika chuo kikuu cha taasisi ya chakula .

  Chuo hicho kikishirikiana na shirika la kimataifa la sheria za chakula kimeripoti kwamba nchini Rwanda wanawake walioshirikishwa kwenye utafiti huo kwa kula maharagwe ya protini ya juu wana fursa kubwa ya kufikiria vyema na kupata madini bora ya mili yao.

  Utafiti huu umefanywa kwa wanafunzi 197 wa vyuo vikuu vya Rwanda na imependekezwa kuwepo kwa sheria za kuhamasisha utumiaji wa maharagwe aina hiyo.

  Dr Mecy Lungaho mtaalamu wa masuala ya lishe bora amesema mwanamke anaekula maharagwe hayo anaweza kufikia mara 5 zaidi ya Yule amabe hajakula.

  Wakulima na wafanyibiashara wanatarajia kupata faida kubwa Rwanda kwani maharagwe hayo sasa yatanunuliwa kwa wengi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako