• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa Zimbabwe awaapisha mawaziri wapya

  (GMT+08:00) 2017-12-04 19:16:21

  Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe leo amewaapisha mawaziri wapya wanaounda baraza la mawaziri, manaibu wao, na mawaziri wa nchi wanaoshughulikia masuala ya mikoa.

  Hafla ya kuapishwa mwaziri hao walioteuliwa alhamis wiki iliyopita imefanyika leo ikulu mjini Harare. Alizungumza na waandishi wa habari baada ya hafla hiyo, rais Mnangagwa amesema serikali ya mpito itakuwa madarakani kwa muda wa miezi saba. Amesema wananchi wa Zimbabwe wanataka umoja na kukuza uchumi wa nchi hiyo.

  Rais Mnangagwa amechukua madaraka wakati hali ya uchumi nchini Zimbabwe ikiwa ni mbaya na nchi hiyo ikikabiliwa na uhaba wa fedha, uwekezaji mdogo wa moja kwa moja wa kigeni, na ukosefu wa ajira.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako