• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Japan kufanya mkutano wa masuala ya bahari

    (GMT+08:00) 2017-12-04 19:17:48

    Mkutano wa ngazi ya juu kuhusu masuala ya bahari kati ya China na Japan utafanyika mjini Shanghai, China, kuanzia kesho.

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Geng Shuang amesema, maofisa kutoka wizara za mambo ya nje, ulinzi, na idara za kutekeleza sheria na usimamizi kutoka nchi hizo mbili watahudhuria mkutano huo wa siku mbili.

    Amesema China inategemea kubadilishana maoni na Japan kuhusu masuala ya bahari yanayofuatiliwa na nchi hizo, kwa lengo la kuimarisha uelewa na kuaminiana.

    Mazungumzo ya mwisho kati ya nchi hizo mbili yalifanyika Fukuoka, Japan, mwezi Juni mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako