• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Polisi nchini Misri wawaua magaidi watano katika mkoa wa Sharqiya

    (GMT+08:00) 2017-12-05 08:47:32

    Wizara ya mambo ya ndani ya Misri imesema jumla ya magaidi watano wameuawa walipopambana na vikosi vya polisi katika mkoa wa Sharqiya. Taarifa iliyotolewa na wizara hiyo inasema magaidi wengine sita walikamatwa kwenye operesheni hiyo iliyofanywa kwenye eneo la jangwa kati ya miji ya Ramadhan na Belbis, ambako ni maficho na kituo cha mafunzo cha magaidi hao. Misri imeshuhudia wimbi kubwa la mashambulizi ya kigaidi yaliyosababisha vifo vya mamia ya polisi na askari, tangu jeshi la nchi hiyo kumwondoa madarakani aliyekuwa rais wa nchi hiyo Mohamed Morsi mwezi Julai mwaka 2013.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako