• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Somalia yakubali kutoa mpango wa mpito kabla ya kuondoka kwa kikosi cha AU

    (GMT+08:00) 2017-12-05 09:22:36

    Somalia imekubali kuweka mpango wa mpito mara moja kwa uungaji mkono wa jumuiya ya kimataifa, kabla ya kuondoka kwa kikosi cha Umoja wa Afrika.

    Wajumbe wanaohudhuria mkutano kuhusu usalama wa Somalia wamekubali kuwa kazi itaanza mara moja ya kuandaa mpango wa kipindi cha mpito unaozingatia hali halisi, wenye hatua mbalimbali na unaofuata ratiba ya kukabidhi majukumu ya kulinda usalama kwa kikosi cha usalama cha Somalia kutoka AMISOM.

    Taarifa ya pamoja inasema kwa hatua ya kwanza, pande zote zitatoa mchakato wa mpango wa mpito mpaka tarehe 31 Desemba, kwa mtazamo wa kukamilisha muswada wa mpango wa mpito kabla ya kufanyika kwa tathmini ya pamoja ya AMISOM, inayotakiwa na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa mwaka 2018.

    Mkutano huo umehudhuriwa na wajumbe wa serikali kuu na wa majimbo, Umoja wa Afrika, Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya na wadau wengine wa kimataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako