• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA, CECAFA: Burundi waitoa jasho Uganda, 0-0

  (GMT+08:00) 2017-12-05 09:47:57
  Timu ya taifa ya Burundi (Intamba Mu-Rugamba), jana imewalazimisha sare ya bila kufungana mabingwa watetezi wa kombe la CECAFA Uganda, kwenye mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa bhukungu mjini Kakamega.

  Alimanusura, Burundi waweke rekodi ya kuifunga Uganda baada ya mpira uliopigwa na Hussein Shaban katika dakika ya 89 kuokolewa na mlinzi wa Uganda Cranes Nikolas Wadada kuuokolea kwenye mstari.

  Mechi nyingine katika kundi hilo inapigwa leo baina ya timu ya taifa ya Ethopia na Sudan Kusini, lakini kwa upande wa kundi A, mechi mbili zitachezwa leo, ambapo Zanzibar Heroes itacheza dhidi ya Rwanda na Libya wataumana na Kenya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako