• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Simanzi Michezoni: Polisi wafanya uchunguzi kifo cha mchezaji Colombia

  (GMT+08:00) 2017-12-05 09:49:00
  Polisi nchini Colombia wanaendelea na uchunguzi dhidi ya kifo cha bingwa wa nchi hiyo kwenye mchezo wa kunyanyua vitu vizito nchini Edwin Mosquera Roa.

  Inadaiwa kuwa Mosquera ambaye amewahi kulitumikia jeshi la nchi hiyo kwa miaka 14 aliuawa kwa kupigwa risasi mjini Palmira.

  Mosquera amefariki akiacha rekodi ya kuwa moja ya wanamichezo maarufu nchini Colombia na duniani kwa ujumla, na kumbukumbu yake ya kimataifa ya hivi karibuni ni pale aliposhika nafasi ya saba kwenye michezo ya Olimpiki mwaka 2016 nchini Brazil.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako