• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Sanamu la Usain Bolt: Serikali ya Jamaica yamshukuru kwa mchango wake 

  (GMT+08:00) 2017-12-05 09:49:40
  Serikali ya Jamaica imeeleza sababu za kutengeneza sanamu la mwanariadha Usain Bolt na kisha kuliweka katika lango kuu la uwanja wa taifa wa michezo wa Kingston.

  Waziri Mkuu wa nchi hiyo Andrew Holmes ambaye ndiyo aliyeongoza zoezi la uzinduzi wa sanamu hilo, ameweka wazi kuwa, mchango wa Bolt katika kuitangaza Jamaica ni mkubwa, hivyo alama hiyo ndiyo shukrani pekee kwake, na kumbukumbu hiyo inafaa kubaki miaka yote ijayo kama ilivyo kwa mashujaa wengine.

  Kwa upande wake, Bolt mwenye rekodi ya dunia ya kushinda medali za dhahabu mara tatu mfululizo katika michezo ya olimpiki kwenye mbio za mita 100, mita 200 na mita 100 katika kupokezana vijiti, hakuwa na neno la kuzungumza zaidi ya kutoa shukrani kwa serikali na watu wa Jamaica.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako