• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa mtandao wa internet duniani watoa ripoti ikionesha mwelekeo mpya wa maendeleo ya sekta hiyo

    (GMT+08:00) 2017-12-05 16:28:19

    Mkutano wa nne wa mtandao wa internet duniani unaofanyika mjini Wuzhen, Zhejiang China umetoa ripoti ya mwaka huu ya maendeleo ya mtandao wa internet duniani, na ripoti ya mwaka huu ya maendeleo ya mtandao wa internet ya China, na pia kutoa orodha ya nchi na makundi mapya ya kiuchumi 38 duniani kuhusu kiwango cha maendeleo ya mtandao wa internet.

    Ripoti ya mwaka 2017 ya maendeleo ya mtandao wa internet duniani imeonesha hali mpya ya maendeleo ya mtandao wa internet ya mabara matano na nchi kuu duniani. Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jana, mkuu wa taasisi ya mtandao wa internet ya China Bw Yang Shuzhen anasema ripoti hii inalenga kutathmini hali ya jumla na hali ya mtu mmoja mmoja kuhusu maendeleo ya mtandao wa internet ya nchi, na inasaidia kupima kiwango cha jumla cha maendeleo ya mtandao wa internet kwa ujumuishi na usahihi.

    "Katika kupima kiwango cha maendeleo ya mtandao wa internet duniani, tumeweka mambo sita, miundombinu, uwezo wa uvumbuzi, maendeleo ya sekta, matumizi ya mtandao wa internet, usalama wa mtandao wa internet na usimamizi wa mtandao wa internet, upimaji wetu unalenga hali ya jumla ya nchi na hali ya mtu mmoja mmoja katika nchi na makundi mapya ya kiuchumi 38 duniani."

    Nchi hizo 38 zinajumuisha nchi sita za Amerika, nchi 13 za Asia, nchi 14 za Ulaya, nchi moja ya Oceania na nchi nne za Afrika. Takwimu zinaeonsha kuwa Marekani, China, Korea Kusini, Japan na Uingereza zinashika nafasi tano za mwanzo. Kwa ujumla, nchi zilizoendelea ziko mbele kwa maendeleo ya mtandao wa internet, zikifuatwa na nchi za Ulaya na Asia. Hata hivyo, nchi za Amerika na nchi za Afrika kusini mwa Sahara zinaongeza juhudi o za kukuza sekta ya mtandao wa internet.

    Ripoti nyingine imepitia hali ya maendeleo ya mtandao wa internet ya China katika miaka mitano iliyopita, na kuonesha uzoefu wa China katika kusimamia mtandao wa internet. Mkuu wa taasisi ya mtandao wa internet ya China Bw Yang Shuzhen anasema,

    "Tumefanya uchambuzi wa kisayansi na tathmini ya kitakwimu kuhusu ufanisi na kiwango cha maendeleo ya mtandao wa internet katika mikoa na miji mbalimbali nchini China katika mambo sita ya miundombinu, uwezo wa uvumbuzi, maendeleo ya sekta, matumizi ya mtandao wa internet, usalama wa mtandao wa internet na usimamizi wa mtandao wa internet. Tumebainisha malengo ya kimkakati na kazi muhimu kuhusiana na maendeleo ya mtandao wa internet kwa mikoa na miji hiyo, na kutaka kutumia nguvu zao bora za kulinganisha, kijiografia na maendeleo, kuinua kiwango cha maendeleo na usimamizi wa mtandao wa internet."

    Ripoti inaonesha kuwa mkoa wa Guangdong, mji wa Beijing, mikoa ya Zhejiang, Jiangsu na mji wa Shanghai inashika nafasi tano za mwanzo. Pia imeonesha kuwa idadi ya wanamtandao wa internet inaongoza duniani, ukubwa wa uchumi wa kidijitali unashika nafasi ya pili duniani, na mauzo ya rejareja katika mtandao wa internet yanaongoza duniani.

    Ripoti ya mwaka 2017 ya mtandao wa internet duniani pia imesema akili bandia imekuwa kitu kipya kwa ushindani wa teknolojia duniani, na uchumi wa kidijitali umekuwa nguvu mpya ya msukumo kwa nchi mbalimbali katika kuhimiza ukuaji wa uchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako