• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wauguzi na wakunga nchini Uganda wafuta mgomo wao

    (GMT+08:00) 2017-12-05 17:44:46

    Wauguzi na wakunga kwenye hospitali za serikali nchini Uganda wamefuta mgomo wao uliopangwa kuanza leo kutokana na madai ya kuongezewa mshahara.

    Taarifa iliyotolewa na ofisi ya waziri mkuu imesema, viongozi wa wahudumu hao wa afya walifanya maongezi na serikali na kukubali kuendelea na mazungumzo kuhusu nyongeza ya mshahara kwa wafanyakazi, badala ya kufanya maandamano. Pande zote mbili zimetoa muda mpaka jumamosi wiki hii kufikia suluhisho la suala hilo.

    Wauguzi na wakunga walipanga kuanza mgomo wao leo kwa madai ya nyongeza ya mshahara na mazingira mabaya ya kazi katika sekta ya afya ya jamii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako