• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Utafiti unaonyesha kuwa wateja wana imani na bidhaa za China

    (GMT+08:00) 2017-12-05 18:41:36

    Utafiti uliofanywa na gazeti la "China Youth Daily" umeonesha kuwa, asilimia 84.1 ya watu wana imani na maendeleo ya bidhaa zinazotengenezwa China.

    Utafiti huo uliofanywa kwa watu 2,012, umeonesha kuwa nguo ni bidhaa inayoongoza nchini China, ikifuatiwa na bidhaa za matumizi ya kila siku, viatu, kofia, na vifaa vya nyumbani.

    Asilimia karibu 60 ya watu waliohojiwa wamekubali kuwa bei nzuri ni kivutio kikubwa cha bidhaa zinazotengenezwa China, na asilimia 48 wamesema chapa za China zinaaminika.

    Karibu nusu ya watu waliohojiwa wamesema ukosefu wa ushindani mkali na ulinzi dhaifu wa hakimiliki ya ubunifu ni vikwazo kwa maendeleo ya kimataifa ya bidhaa za China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako