• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la biashara la China na Afrika lapenda kuhimiza maendeleo ya uwekezaji na biashara kati ya pande hizo

    (GMT+08:00) 2017-12-05 19:04:41

    Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya baraza la biashara la China na Afrika Bw. Wang Licheng amesema, mwaka kesho mkutano wa 7 wa mawaziri wa baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC utafanyika hapa China, na baraza la biashara la China na Afrika litatumia fursa hiyo kuhimiza maendeleo ya uwekezaji na biashara kati ya pande hizo mbili.

    Bw. Wang amesema hayo alipohutubia kongamano la uchumi, biashara na uwekezaji la ushirikiano kati ya China na Afrika na pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" uliofanyika jana hapa Beijing. Amesema, chini ya utaratibu wa FOCAC na Pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja", China na Afrika zina msingi imara na nguvu kubwa ambazo hazijatumiwa ipasavyo za ushirikiano, na pande hizo mbili zote zinataka kuhimiza ushirikiano na kuunganisha mikakati ya kitaifa katika uzalishaji wa kiviwanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako