• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania-Wakulima wa tumbaku waonywa kutolima zaidi ya kilo milioni 8

  (GMT+08:00) 2017-12-05 20:21:02

  Wakulima wa tumbaku wilayani Kahama,nchini Tanzania wametahadharishwa kuheshimu mkataba wa kampuni za ununuzi ili kusitokee msukosuko wowote.

  Msimu uliopita kilo milioni tatu zilikosa soko.

  Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirikia (Kacu) Bw Emmanuel Peter amesema mwaka huu wakulima wameingia mkataba na kampuni za ununuzi kuzalisha kilo milioni nane za tumbaku ,hivyo wanapaswa kulima bila kuzidi.

  Mwaka jana tumbaku iliyozidi kwa Kahama ilikuwa kilo milioni 3.25 ambayo ilikuwa ni ziada ya mkataba wa kuzalisha kilo milioni sita ambazo kampuni ziligoma kununua ziada hiyo.

  Wanunuzi wakuu wa zao hilo ni kampuni ya TLTC na Alliance One.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako