• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania-Uchunguzi wa mafuta na gesi katika vitalu vya Pemba,Zanzibar wakamilika

  (GMT+08:00) 2017-12-05 20:22:28

  Mkurugenzi mwendeshaji wa mamlaka ya udhibiti wa utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia Omar Zubeir amesema uchunguzi wa utafutafutaji wa rasilimnali hiyo katika eneo la bahari yenye maji ya kina kirefu limefanikiwa licha ya changamoto.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana,alisema uchunguzi huo umeonyesha matumaini ya kupatikana kwa mafuta.

  Alisema uchunguzi ulianza Oktoba 28 na kumalizika Novemba 28 mwaka huu.

  Alisema idadi ya mistari iliyofanyiwa utafiti ndani ya kitalu cha Pemba ilikuwa 62,huku idadi ya kilomita zilizofanyiwa utafiti ndani ya kitalu cha Pemba zilikuwa 2,482.

  Aidha alisema idadi ya mistari iliyofanyiwa utafiti nje ya kitalu Pemba,Zanzibar ilikuwa ni minne huku idadi ya kilomita zilizofanyiwa utafiti nje ya kitalu cha Pemba,Zanzibar zilikuwa 333.6.

  Alisema katika uchunguzi huo changamoto zilizojitokeza ni kuwapo kwa wavuvi katika baadhi ya maeneo,ambao walisababisha uchunguzi kusimama kwa muda ili kupisha shughuli za uvuvi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako