• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya-Viwanda vyatengeza mifuko ya plastiki licha ya marufuku

  (GMT+08:00) 2017-12-05 20:23:06

  Utengezaji wa mifuko ya plastiki bado unaendelea nchini Kenya zaidi ya miezi mitatu baada ya kupigwa marufuku.

  Imebainika kuwa wanaotengeza mifuko hiyo kinyemela wanapatikana katika eneo la Viwandani jijini Nairobi,Mlolongo katika kaunti ya Machakos na Thika.

  Marufuku ya matumizi ya mifuko ya palstiki ilianza tarehe 28 mwezi wa Agosti,hii ikimaanisha kuwa yeyote atakayepatikana akiuza,akitengeza au akibeba mifuko ya palastiki atatozwa faini ya hadi shilingi milioni 4 au kufungwa jela kifungo cha hadi miaka minne.

  Mamlaka ya Usimamizi wa Mazingira nchini Kenya (Nema)imesema itaongeza ufuatiliaji kuhusu utengenezaji wa mifuko ya palstiki kinyemela.

  Naibu Mkurugenzi wa mamlaka ya NEMA ,Ali Mwanzei amesema wenye viwanda viwili tayari wamekamatwa kwa kuendelea kutengeza mifuko ya plastiki.

  Vyanzo vinadokeza kuwa takribana viwanda 20 vya utengezaji plastiki vinafanya kazi kinyume cha sheria jijini Nairobi,ikiashiria udhaifu katika utekelezaji wa marufuku hiyo wakati wafanyabiashara wakiendelea kukiuka amri.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako