• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanamazingira walioanzisha misitu ya Saihanba wapewa tuzo ya walinzi wa dunia ya Umoja wa mataifa

    (GMT+08:00) 2017-12-06 09:12:09

    Shirika la mpango wa mazingira la Umoja wa mataifa UNEP jana mjini Nairobi lilitangaza kutoa tuzo ya walinzi wa dunia ya Umoja wa mataifa kwa wanamazingira walioanzisha misitu ya Saihanba, kaskazini mwa mkoa wa Hebei, China.

    Misitu ya Saihanba yenye eneo la hekta elfu 93 ilianzishwa kwenye sehemu zilizokuwa zinakabiliwa na hatari ya kubadilika kuwa jangwa kutokana na ukataji ovyo wa miti. Kuanzia mwaka 1962, mamia ya wanamazingira walianza kupanda miti kwenye eneo hilo, na baada ya juhudi za vizazi vitatu, kiwango cha eneo la misitu kwenye sehemu hiyo kimeongezeka kutoka asilimia 11.4 hadi asilimia 80.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako