• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Utawala bora umetajwa kuleta msukumo mkubwa kwa mageuzi barani Afrika

    (GMT+08:00) 2017-12-06 09:51:52

    Wataalamu na watunga sera barani Afrika wamesisitiza kuwa utawala bora unatoa msukumo mkubwa kwenye mageuzi ya kuhimiza maendeleo ya uchumi, na mchakato wa kuleta demokrasia barani Afrika.

    Wataalamu hao wamesema hayo kwenye mkutano kuhusu uchumi wa Afrika kwa mwaka huu, unaofanyika huko Addis Ababa. Kwenye mkutano huo waziri mkuu wa Ethiopia Bw Hailemariam Desalegn, amewaambia washiriki kuwa utawala bora unachochea mageuzi, maendeleo na mchakato wa demokrasia, na Afrika haiwezi kupoteza fursa hii ya kuufanyia mageuzi uchumi wake ili kuwanufaisha watu wake.

    Amesema kuwa kazi nyingi zinazohitaji nguvu kazi kubwa zinaondoka kutoka kwenye nchi zilizopata maendeleo ya kiviwanda na kwenye masoko mazuri ya ajira, hii ni fursa kwa bara la Afrika kujiondoa kwenye taabu na kuwa nyuma.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako