• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kikapu: Timu ya CSK yajiondoa kwenye ligi kuu Rwanda

  (GMT+08:00) 2017-12-06 10:45:01
  Mabingwa wa zamani katika ligi kuu ya mchezo wa mpira wa kikapu nchini Rwanda, klabu ya Cercle Sportif de Kigali (CSK), imetangaza kujiondoa katika mashindano hayo kwa msimu huu.

  Kwa mujibu wa katibu mkuu wa klabu hiyo, Jean Luc Mugabo, kamati hiyo imeamua kufanya hivyo kutokana na hali ya kiuchumi ya klabu hiyo kutokuwa ya kuridhisha, ambayo iliipelekea kupata matokeo mabaya msimu uliopita.

  Kwa mujibu wa katibu huyo CSK, inatarajiwa kukosekana kwa msimu mmoja tu, ambapo wakati wa mapumziko ikitarajiwa kuweka mipango ya muda mrefu na kurejesha hadhi na heshima ya timu hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako