• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Olimpiki: Timu ya Taifa ya Urusi yazuiwa kushiriki katika majira ya baridi Korea Kusini

    (GMT+08:00) 2017-12-06 10:45:20
    Timu ya taifa ya Urusi imezuiwa kushiriki mashindano ya olimpiki ya majira ya baridi yatakayofanyika mwakani mjini Pyeongchang nchini Korea Kusini.

    Lakini licha ya kifungo hicho, wachezaji wa Urusi ambao watakuwa tayari kupimwa na wakathibitika kutotumia dawa zilizokatazwa michezoni, basi wataruhusiwa kushiriki kama wachezaji huru wasiokuwa na bendera ya utaifa.

    Uamuzi huo uliochukuliwa na kamati ya kimataifa ya Olimpiki, umepingwa vikali na maofisa wa ngazi za juu Urusi wakiwemo wanasiasa ambao wamepanga kuitisha mgomo kuhusu michezo hiyo.

    Mvutano huu baina ya Urusi, kamati ya kitaifa ya Olimpiki ROC na kamati ya kimataifa ya Olimpiki umetokana na shutuma za muda mrefu za Urusi kukaidi sheria na mfumo wa ukaguzi wa kimatifa wa matumizi ya dawa za kuongeza nguvu michezoni.

    Michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi ya Korea Kusini inatarajiwa kuanza Februari 9, mwaka 2018.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako