• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Reli ya mwendo kasi kati ya miji miwili ya China magharibi yazinduliwa

    (GMT+08:00) 2017-12-06 16:53:46

    Reli ya treni ya mwendo kasi inayounganisha mji wa kaskazini magharibi wa China Xi'an na mji wa kusini magharibi wa China Chengdu imezinduliwa leo, ikipunguza muda wa usafiri kati ya miji hiyo miwili kutoka saa 11 hadi saa 4 tu. Treni ya mwendo kasi ya kwanza iliondoka Xi'an, mji wa mkoa wa kaskazini magharibi wa China Shaanxi leo asubuhi, na kusimama katika vituo 14 kabla ya kufika Chengdu, mji wa mkoa wa Sichuan.

    Ikiwa imesanifiwa kwa mwendo wa kilomita 250 kwa saa, treni hiyo itapunguza muda wa usafiri kati ya miji hiyo miwili hadi saa nne na dakika 7. Na muda huo utapunguzwa hadi saa tatu na dakika 27 hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu.

    Reli hiyo mpya yenye urefu wa kilomita 658 ni reli ya kwanza nchini China kupitia milima ya Qinling, ambayo ni mpaka wa kimaumbile kati ya kaskazini na kusini mwa China. Ikitumiwa kama kizuizi cha kimaumbile cha ulinzi katika zama za kale, milima ya Qinling inajulikana kwa ardhi yake yenye mabonde na barabara zenye hatari. Hii ni changamoto kubwa kwa dereva anayeendesha treni hiyo. Anayesimamia mambo katika kipande cha Xi'an cha reli hiyo Zhang Kejun anasema,

    "Madereva wamefanya majaribio mara kwa mara katika kuendesha treni hiyo ya mwendo kasi, ili wasafiri wasijisikie athari mbaya inayotokana na reli hiyo, na kuona kama treni inaendeshwa katika reli iliyonyooka."

    Reli ya Xi'an-Chengdu inapita katika mahandaki mengi yanayochukua asilimia 55, pamoja na athari ya milima ya Qinling, mawasiliano ya simu yalikabiliwa na matatizo. Na ili kuwawezesha wasafiri wawasiliane na nje katika treni hiyo, vifaa vya 4G vimewekwa katika reli hiyo. Naibu meneja wa kampuni ya China Tower tawi la mkoa wa Shaanxi Bw Wang Bao anasema,

    "Kupitia kufunika kwa huduma za mtandao za 4G katika usafiri mzima wa reli hiyo, wasafiri wanaweza kutembelea tovuti, kupiga simu ya video kutumia internet, na pia kuona video yenye hali ya juu ya picha mtandaoni. Na bila shaka kupiga simu kupitia mtandao hakuna tatizo lolote."

    Hivi sasa, kila siku treni 7 zinafanya safari ya kutoka Xi'an hadi Chengdu na treni nyingine 7 zinatoka Chengdu hadi Xi'an. Wataalamu wanaamini kuwa reli hiyo ya mwendo kasi itaimarisha mtandao wa reli ya mwendo kasi wa China kuunga mkono maendeleo ya China magharibi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako