• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais Xi asema China itatoa fursa na mchango zaidi kwa dunia

  (GMT+08:00) 2017-12-06 17:58:20

  Rais Xi Jinping wa China amesema nchi yake itatoa fursa zaidi na kutoa mchango mkubwa zaidi kwa dunia.

  Rais Xi amesema hayo leo katika barua ya pongezi kwa mkutano wa Baraza la Fortune Duniani ulioanza leo mjini Guangzhou hapa China. Katika barua hiyo, rais Xi amesema China itaendeleza uchumi wa wazi kwa ngazi ya juu, kuhimiza Pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja, na kusukuma mbele muundo mpya wa kufungua mlango kwa pande zote.

  Rais Xi pia amesema, China ina msingi, mazingira na msukumo wa kudumisha ukuaji wa utulivu na wa kasi wa kiuchumi. Ameongeza kuwa, China itaendelea kujenga uhusiano wa wenzi wa kimataifa, kupanua maslahi ya pamoja na nchi nyingine, kuongeza uhuru na kurahisisha biashara na uwekezaji, na kusukuma mbele mafungamano ya kiuchumi ambayo ni ya wazi na jumuishi, yenye usawa, na yanayonufaisha pande zote.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako