• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Serikali ya Rwanda kubadili sheria ya zabuni

  (GMT+08:00) 2017-12-06 19:36:12
  Serikali ya Rwanda imewasilisha bungeni muswada wa kubadili sheria ya zabuni ili bidhaa za nchini humo zipate upendeleo wa angalau asilimia 65 kwenye zabuni za serikali.

  Mabadiliko hayo yana lengo la kuwezesha utekelezaji sera na kampeni ya kuhamasisha kuthamini bidhaa na huduma za nchini humo. Sheria ya sasa inatoa upendeleo wa asilimia 10 kwa bidhaa na huduma za ndani kwa zabuni zinazoshirikisha waombaji kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na nchi wanachama wa Soko la Pamoja la Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (COMESA).

  Kwa mujibu wa Waziri wa Biashara na Viwanda wa Rwanda, Vincent Munyeshyaka, serikali inataka kubadili utaratibu ili bidhaa na huduma za nchini humo zipate upendeleo na kupunguza nguvu ya kampuni za nje kwenye zabuni za serikali.

  Waziri Munyeshyaka alisema, wazalishaji binafsi wanaotengeneza bidhaa nchini humo watapewa fursa muhimu ya kushinda zabuni za serikali, na kwamba, mabadiliko hayo hayataathiri ubora wa bidhaa na huduma.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako