• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa Tanzania akutana na viongozi wa kampuni ya Total

  (GMT+08:00) 2017-12-06 19:36:12
  Rais wa Tanzania John Magufuli amekutana na viongozi wa kampuni ya Total ambayo ni mwekezaji mkubwa wa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi la kutoka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga.

  Katika kikao hicho Rais Magufuli amewahakikishia viongozi hao kuwa Tanzania itatoa ushirikiano wa kutosha kwa kampuni hiyo na washirika wengine katika ujenzi wa mradi huo.

  Rais Magufuli aliitaka Total kuharakisha ujenzi wa bomba hilo uliopangwa kuanza mwezi ujao na kukamilisha mapema hata kabla ya mwaka 2020 ili wananchi wa Tanzania na Uganda waanze kunufaika na mafuta hayo.

  Aliitaka kampuni hiyo kuzingatia kutoa ajira kwa Watanzania katika wilaya 24 ambazo bomba litapita huku akiwahakikishia kuwa Tanzania inao wakandarasi na wahandisi wa kutosha na wenye uwezo wa kushirikiana nao katika ujenzi wa bomba hilo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako