• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • TMEA yazindua kampeni ya uhamasisho kuhusu changamoto wanazopata wajasiriamali wanawake EAC

  (GMT+08:00) 2017-12-06 19:36:12
  Shirika la uwezeshaji biashara la Trademark East Africa (TMEA) limezindua kampeni inayolenga kujenga ufahamu kuhusu changamoto wanazopitia wajasiriamali wanawake katika ukanda wa Afrika Mashariki.

  Kampeni hiyo ya wajasiriamali wanawake itaangazia fursa za biashara kwa wanawake ili kuongeza ujumuishwaji na upatikanaji wa fursa za biashara.

  Chini ya kaulimbiu ya "Kuwawezesha wanawake,kuongeza biashara",kampeni hiyo itafanya TMEA kuwajumuisha watungaji sera,washirika wa maendeleo,vyama vya kibiashara na wadau wengine katika kanda nan je kujenga mazingira bora kwa wafanyabiashara wanawake.

  Afisa Mkuu Mtendaji wa TMEA Frank Matsaert amesema awamu ya kwanza ya mpango huo imewanufaisha wanawake 25,000 wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako