• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zaidi ya wakulima 2,000 Tanzania  wamepewa mbegu za alizeti

    (GMT+08:00) 2017-12-06 19:40:48

    Zaidi ya wakulima 2,000 wilayani kahama nchini Tanzania wamepatiwa mbegu za alizeti ili kuongeza mazao ya biashara yaliyokuwapo kukumbwa na magonjwa katika uzalishaji wake.

    Akizungumza kwenye uzinduzi wa jengo la kiwanda cha kukamua mafuta ya alizeti, meneja mkuu wa ushirika wa Ibuka Multipurpose Co-operative Society Ltd, Musiba Mkama alisema kutokana na ugawaji mbegu hizo wanatarajia uzalishaji kuongezeka.

    Kufunguliwa kwa kiwanda hicho kinafanya idadi ya viwanda vinavyosindika mafuta wilayani Kahama kufikia viwili.

    Viwanda hivyo vina uwezo wa kusindika tani 434,725 za alizeti kwa mwaka, wakati hali halisi ya upatikanaji malighafi ni wastani tani 160,000 kwa mwaka hivyo kuwapo upunfufu wa tani 274,725.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako