• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Putin amesema atagombea tena urais mwaka 2018

  (GMT+08:00) 2017-12-07 09:06:52

  Rais Vladmir Putin wa Russia amesema kuwa atagombea awamu mpya ya urais kwenye uchaguzi wa mwaka kesho wa Rais wa Russia. Rais Putin amenukuliwa akisema hayo kwenye kiwanda kimoja cha magari mjini Nizhny Novgorod.

  Uchaguzi mkuu wa Russia umepangwa kufanyika mwezi Machi mwaka kesho, na Rais Vladmir Putin anatarajiwa kupata ushindi mkubwa. Rais Putin alichaguliwa kwa mara ya kwanza kuwa Rais wa Russia mwaka 2000, na kuchaguliwa tena mwaka 2004. Alikuwa waziri mkuu wa Russia kuanzia mwaka 2008 hadi mwaka 2012, na mwaka huo huo alichaguliwa tena kuwa Rais wa Russia.

  Watu kadhaa tayari wametangaza nia ya kugombea urais ikiwa ni pamoja na wagombea kadhaa wa vyama vya upinzani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako