• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • EPL: Jose Mourinho amshutumu Pep Gurdiola kwa kutoa tarifa za uongo juu ya majeruhi wake

  (GMT+08:00) 2017-12-07 09:16:44

  Mwishoni mwa wiki hii mchezo mkubwa kabisa wa kufunga mwaka EPL utapigwa kati ya majirani wawili Manchester United watakaokuwa nyumbani kuwakaribisha Manchester City.

  Huu ni mchezo baina ya vilabu viwili vyenye nguvu ya pesa lakini pia ni mchezo kati ya makocha wawili ambao wanatajwa kuwa moja kati ya makocha bora sana duniani katika kizazi cha sasa.

  Hata hivyo tayari Jose Mourinho ameanza maneno kwa kumshutumu kocha wa Manchester City Pep Gurdiola kwamba anadanganya kuhusu majeruhi. Gurdiola alinukuliwa akisema David Silva ni majeruhi na anaweza kukosa mchezo wa Derby, jambo hilo limepokelewa tofauti na Mourinho kwani anaamini sio kweli na Pep anajua kwamba Silva atakuwepo.

  United wanakutana na City ambao msimu huu wanaonekana kuwa tishio kubwa si tu nchini Uingereza bali barani Ulaya kwa ujumla, kama City itashinda mchezo huu itazidi ongeza pengo la alama kati yake na United na United wanahitaji kushinda ili kupunguza pengo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako