• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kombe la Chalenji: Ni ndugu wawili Kili Stars na Zanzibar Heroes

    (GMT+08:00) 2017-12-07 09:17:03

    Timu ya soka ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars leo itakuwa na kibarua kigumu katika michuano ya Kombe la Chalenji wakati watakapokabiliana na ndugu zao wa Zanzibar Heroes, ili kuamua hatima yao ya kutinga nusu fainali.

    Kili Stars inayonolewa na Kocha Ammy Ninje ilianza michuano hiyo kwa sare tasa na Libya katika mechi za Kundi A, hali inayoifanya lazima ishinde leo kwenye Uwanja wa Kenyatta, mjini Machakos.

    Zanzibar Heroes ilianza kwa kishindo michuano hiyo juzi kwa kuichapa Rwanda mabao 3-1 na kuifanya ishike nafasi ya pili nyuma ya wenyeji wao Kenya wanaoongoza msimamo wa kundi lao wakiwa na alama 4.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako